Monday, October 4, 2010
MSAADA
habari za kazi na maisha. Kwanza nakupa hongera kwa kazi nzuri unayoifanya katika kuendeleza blog yako. Pili nakushukuru kwa kupata muda wa kuisoma mail yangu hii, naamini uko busy sana na unapata email nyingi kila siku, kwa hivyo sitochukuwa muda mrefu kueleza malengo ya email hii.
Kwa jina naitwa Ahmed Salem, kwa muda huu ninaishi na kufanya kazi hapa uk. Nilikuja kipindi na kujitahidi kujisomesha wakati huo huo nikipiga boksi. Nimefanikiwa kumaliza masomo yangu na nimekuwa nikifanya kazi katika kampuni moja ya IT hapa london kama Technical Support Field Engineer.
Kwa muda mrefu lengo langu ni kurudi nyumbani na kusaidia wanyonge wenzangu kielimu. Nahisi muda umefika wa mimi kurudi nyumbani na kutimiza lengo langu. Nakusudia kurudi nyumbani mwanzoni mwa mwezi wa januari na nataka kufanya kazi ya kusomesha vijana kwenye charity organisation.
Ninachotaka kuomba kwako na wasomaji wako walio tanzania ni msaada na muongozo wa kuweza kuwasiliana na charity organization zilizopo tanzania ambazo zinawasaidia watoto na vijana kielimu. Ningelipenda zaidi kujua organisation zilizo na base sehemu kama arusha, tanga na visiwani zanzibar.
Nakaribisha, ushauri na mawazo kutoka kwa wote.Pia napokea maoni na ushauri kupitia email hii
ahmedyoungafrican@gmail.com
ahsante sana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Sijui organization nyingi ila kuna organization moja inaitwa SOS wana vituo vyao Dar, Arusha na Zanzibar nafikiri huko Mr. Salem anaweza kufanikisha malengo yake.
Tafuta SOS Tanzania kwenye Google na utapata taarifa zaidi
Post a Comment