Home

HOME I

Thursday, November 4, 2010

Dr Slaa : Matokeo yamechakachuliwa...

 











                          



   Dk Willibrod Slaa.
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa jana alitoa tuhuma nzito dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa akisema kuwa taasisi hiyo imemuibia kura na hivyo hatayakubali matokeo ya uchaguzi wa urais.

Kauli hiyo imetolewa wakati Tume ya Uchaguzi (Nec) ikielekea kukamilisha kutangaza matokeo ya majimbo na kumtangaza mshindi, jambo ambalo litamfanya Dk Slaa na chama chake kuzuiwa na katiba ya nchi kupinga matokeo hayo mahakamani.

Dk Slaa aliwaambia waandishi wa habari jana akisema kuwa: "Kuna uchakachuaji mkubwa wa kura na kazi hiyo inafanywa na Usalama wa Taifa," alisema Dk Slaa ambaye matokeo yanayotangazwa na Nec yanaonyesha kuwa anaendelea kushika nafasi ya pili akiwa nyuma ya mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete.

Lakini Mwenyekiti wa Nec, Jaji Lewis Makame alipoulizwa kuhusu tamko hilo la Chadema, alimtaka Dk Slaa kuwasilisha taarifa zinazothibitisha madai aliyoyatoa kuwa Nec imekuwa ikitangaza matokeo yaliyochakachuliwa tofauti na zile alizopata.

Jaji Makame alisema kama madai ya Dk Slaa ni ya kweli, ni muhimu apeleke hizo idadi ya kura alizodai amepunjwa ili kuthibitisha madai yake dhidi ya tume hiyo.

Alisema idadi ya kura zinazotangazwa na Nec kwenye kinyang’anyiro cha urais ni zile ambazo wagombea hao wamezipata kihalali kwenye upigaji kura na wala hakuna upendeleo wowote.

“Mimi sijapata malalamiko yoyote kutoka kwa mgombea huyo, hivyo kama anayoyazungumza ni ya kweli kuna umuhimu wa kuthibitisha hiyo tofautu anayodai ipo, lakini kura tunazotangaza ni kura ambazo kila mgombea alizipata kwenye uchaguzi," alisema Jaji Makame
Mbunge huyo wa zamani wa Jimbo la Karatu alionya kama Nec inaitakia mema nchi hii, ifute matokeo yote ya urais na uchaguzi urudiwe upya.

"Hatuwezi kukubali matokeo yanayopikwa na Usalama wa Taifa. Hayo si matakwa ya wananchi," alisema Dk Slaa baadaye kukaririwa kwenye TBC.

Kwa mujibu wa Dk Slaa, ambaye pia ni katibu mkuu wa Chadema, chama chake kimekuwa kikifuatilia kwa makini matokeo hayo na kugundua wizi mkubwa wa kura kwenye nafasi za urais na ubunge.

Mgombea huyo wa urais, ambaye mara nyingi hujenga hoja kwa kutumia ushahidi, alisema moja ya maeneo waliyogundua kuwepo kwa wizi wa kura ni matokeo ya Jimbo la Geita lililo mkoani Mwanza ambako alidai Nec ilitangaza kuwa kwenye uchaguzi wa rais, CCM imepata kura 17,792 na Chadema kura 3,789.

Lakini akasema kwa mujibu wa fomu walizonazo ambazo zilisainiwa na mawakala wao kwenye kata 20 za jimbo hilo, CCM ilipata kura 30,960 na Chadema 15,736.

"Nashangaa Nec wanatangaza matokeo haya kutoka wapi? Hayo ya Geita ni moja tu. Kule Hai, fomu zinaonyesha kwenye urais CCM ina kura 20,120 na Chadema 26,724, lakini Nec imetangaza kuwa CCM ina kura 35,910 na Chadema kura 18,513," alisema Dk Slaa huku akionyesha baadhi ya fomu kwa waandishi wa habari.

Dk Slaa pia alitoa mfano aliodai kuwa wizi wa kura katika kituo namba 00070103 cha Ubungo jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa fomu 24A inaonyesha CCM wamepata kura 68,727 na Chadema 65,450, lakini matokeo ya kata za Ubungo yanaonyesha CCM ina kura 70,472 na Chadema 72,252.

Dk Slaa alisema mbali na Ubungo, tatizo hilo pia alidai liko Kigoma Mjini ambako Chadema imeshinda kwa zaidi ya kura 500, lakini "matokeo yalichakachuliwa na kusababisha vurugu hadi askari wakawapiga mabomu wafuasi wa Chadema".

Pia alisema kwenye Jimbo la Segerea, ambako matokeo yalicheleweshwa kwa siku mbili na kutangazwa usiku wa manane juzi, mambo ni mabaya zaidi kwa kuwa fomu 21 A na B hazikuwepo na wasimamizi walikwenda nazo majumbani kulala.

"Kiwalani fomu hazikuwepo na matokeo hayakuonekana. Kipawa vituo vinne matokeo hayakuonekana na Vingunguti kuna vituo saba na Tabata vituo viwili ambako matokeo hayakuonekana," alisema Dk Slaa.

Aliongeza kusema: "Hali kama hiyo pia imetokea Morogoro Mjini. Matokeo hayajaonekana na yametangazwa tu. Kibakwe na Kiteto mgombea hakushirikishwa katika kutangaza matokeo.

"Hayo ni majimbo ya mifano tu. Yapo majimbo mengi na kutokana na hali hiyo, Chadema imetoa tahadhari kwa Tume na vyombo vya ulinzi na usalama kuwa taratibu hazijafuatwa na nyingi zimevunjwa."

Dk Slaa alisema kuwa ni muhimu waangalizi wote wa uchaguzi wakatoa taarifa zao hadharani ili kusaidia nchi na kumtaka mkuu wa Jeshi la Polisi kuendesha chombo hicho cha dola kwa haki na maadili waliyosaini.
Baadaye mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa kauli hiyo ya Dk Slaa ni tamko rasmi la Chadema.

Akizunguzia ucheleweshaji wa mataokeo unaodaiwa kutokea kwenye majimbo ambayo CCM imeonekana kukabwa koo na vyama vyama vya upinzini, Jaji Makame alisema wao wanatangaza matokea wanayopelekewa na wala hakuna ucheleweshaji wowote.

Mkuu wa kitengo cha uchaguzi cha CCM, Mattson Chizi alisema hoja za Dk Slaa zimejikita kwenye matokeo yanayotangazwa na Nec hivyo hawezi kuzungumzia suala hilo.
"Tunachosubiria ni matokeo ya jumla na hatuwezi kuingilia kazi ya tume," alisema.

Kwa upande wa CUF, Meneja wa Kampeni wa chama hicho, Said Miraji, alisema aligoma kuzungumzia suala akieleza kwamba CUF kitaandaa taarifa kuhusu uchaguzi ambayo itatolewa baadaye na mgombea urais wao, Prof Ibrahim Lipumba.


CHANZO: MWANANCHI

Tuesday, November 2, 2010

MR II a.k.a SUGU ASHINDA UBUNGE MBEYA MJINI

Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Joseph Mbilinyi aka MR II (Sugu ) ameshinda uchaguzi wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA kwa kumbwaga vibaya mgombea wa CCM na wagombea wengine.


MR II alishinda uchaguzi wa Mbeya Mjini kwa kuwabwaga vibaya wapinzani wake, Benson Mpesya wa CCM, Prince Mwaihojo, wa CUF, Tokolasi Kasuluari wa DP na Aggabo Mwakatobe wa NCCR.

Msimamizi wa jimbo hilo alimtangaza MR II kuwa ni mshindi wa jimbo hilo baada ya kupata kura 46,411 huku mpinzani wake mkubwa toka CCM, Benson Mpesya akifuatia kwa mbali akiwa na kura 24,327.

Freeman mbowe warudi bungeni na Augustino lyatonga mrema


 
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe ameshinda uchaguzi Jimbo la Hai na kurejea bungeni tena kama mbunge baada ya kuwa nje kwa miaka mitano
 
 Mwenyekiti wa TLP Mh. Augustino Lyatonga Mrema  ametangazwa kuwa Mbunge mteule wa Jimbo la Vunjo baada ya kushinda kwenye kinyang'anyiro cha kiti hicho baada ya kukaa nje kwa muongo mmoja
 
 

Rais mpya wa zanzibar ni Dk Ali mohamed shein

Rais Mteule, Dk. Shein kupitia CCM ameshinda kwa jumla ya kura 179, 809 sawa na 50.1% ya kura zote, il hali Maalim Seif kupitia CUF amepata kura 176, 538 sawa na 49.1% na zilizobaki ni za vyama vingine.

Maalimu Seif pia ameipongeza tume ya uchaguzi ya Zanzibar, ZEC, kwa zoezi la uchaguzi, lakini pia ametoa maoni juu ya mapungufu aliyoyaona hasa kuhusu shahada za kupiga kura na matumizi ya mabavu kwa mawakala wa vyama na watu mbalimbali wanapohoji na kutaka taarifa sahihi. Amemsihi Rais Mteule alishughulikie suala hilo. Kabla ya kuhitimisha hotuba yake fupi, Malim Seif alisema kuwa katika matokeo haya, "hakuna mshindi wala mshindwa" kwani washindi ni Wazanzibari na imani yake ni kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa italeta mafanikio nchini humo. Amemsihi Rais Mteule kuwaasa watu kuacha kubezana, kwani kufanya h ivyo kunaweza kusabababisha mtafaruku. Baada ya kuzungumza, Malim Seif alinyanyuka na kumpa mkono wa pongezi Rais Mteule wa Zanzibar, 2010 - 2015, Dk. Ali Mohamed Shein.

Ilipofika zamu ya Rais Mteule kuzungumza, naye alitoa pongezi kwa Maalim Seif na kupongeza zoezi zima la uchaguzi jinsi lilivyoendekea. Pia ametoa ahadi ya kushirikiana na wote katika ujenzi wa Zanzibar mpya kwa mujibu wa maridhiano mapya ya uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar.

Monday, November 1, 2010

Masha, Batilda, Mramba, Mkuchika mambo magumu

 
Mwenendo wa matokeo ya awali yaliyokuwa yakikusanywa hadi jana usiku yameonyesha kuwa vigogo takribani wagombea 10 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wana hali ngumu.Taarifa zilizokusanywa na Mwananchi katika majimbo mbalimbali zinaonyesha kuwa Philip Marmo (Mbulu), Lawrance Masha (Nyamagana), Dk Batilda Buriani (Arusha Mjini), Kapteni George Mkuchika (Newala) na Basil Mramba (Rombo) hali zao ni ngumu katika uchaguzi huu.

Matokeo yalikusanywa katika kata za majimbo ya wagombea hao yanaonyesha kwamba kuna mchuano mkali sana baina yao na wale wa vyama vingine na baadhi yao wamezidiwa hadi zaidi ya nusu ya kura, huku kata zilizobaki katika majimbo hayo zikiwa ni za kunyang'anyana.

Washindani wakubwa wa wagombea hao wanatoka CHADEMA na CUF ambavyo vimeweza kuongeza ushawishi katika maeneo mbalimbali nchini, kubwa ikiwa ahadi yao ya kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita.

Hadi jana jioni mvutano ulikuwa mkali katika majimbo hayo huku askari wa jeshi na wale wa polisi wakijaribu kutuliza hali ya mvutano uliokuwa umeanza kujikita kwenye majimbo hayo.

Taarifa zaidi zilieleza ukiukwaji wa taratibu wakati wa kura za maoni, tuhuma za rushwa na wanachama kupinga maamuzi ya baadhi ya kamati za siasa za mikoa kugeuza matokeo, ni mambo ambayo yanaendelea kuisumbua CCM.

Matokeo mengine ya awali ya urais, ubunge na udiwani yalionyesha jimbo la Simanjiro Kata ya Ngorika kura za urais CCM imepata kura 853, CHADEMA 282, CUF 5, APPT 3 na NCCR 1. Udiwani katika Kata hiyo CCM imepata kura 941 na CHADEMA 200.

Katika Kata ya Kibaya jimbo la Kiteto, kura za urais CCM imepata 83, CHADEMA 102 na CUF kura 4. Katika ubunge CHADEMA imepata kura 132, CCM 60 na CUF 2. Kwa upande wa udiwani CHADEMA imepata kura 125 na CCM 67.

Katika Kata ya Sanya Juu jimbo la Siha CCM imepata 1,269 na CHADEMA 949.

Kata ya Ngamiani Kusini, urais APPT 3, CCM 1,145, CHADEMA 104, CUF 1,254 na NCCR 4 udiwani CCM 11,180, CHADEMA 52, CUF 1,479 na UDP 5. Ubunge  jimbo la Lupa, CCM 1,039, TLP 589, CHADEMA 37 na CUF 5.

Source: Mwananchi

matokeo ya urais yazidi kutangazwa majimboni

Picture
Lewis Makame - NEC Tanzania
MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO JIMBO: SIHA

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 241 (1.02% )
KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 15,570 (65.69% )
SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 7,226 (30.49% )
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 83 ( 0.35% )
RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 18 ( 0.08% )
MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 11  (0.05% )
DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 14 ( 0.06% )
SPOILT VOTES 538 2.27% TOTALS 23,701 100.00%
----------------------------

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO JIMBO: MPANDA VIJIJINI

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 128 ( 1.03% )
KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 7,817 (62.87% )
SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 3,669 (29.51% )
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 378 (3.04% )
RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 26 (0.21% )
MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 17 ( 0.14% )
DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 13 ( 0.10% )
SPOILT VOTES 386 3.10% TOTALS 12,434 100.00%
----------------------------

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO JIMBO: LONGIDO

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO   (0.77% )
KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 17,066 (83.64% )
SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 2,702 (13.24% )
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 114  (0.56% )(
RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 10 )0.05%
MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 4 ( 0.02% )
DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 7 (0.03% )
SPOILT VOTES 344 1.69% TOTALS 20,404 100.00%
----------------------------

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO JIMBO: CHILONWA

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 319 (1.35% )
KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 19,780 (83.68% )
SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 2,439 (10.32% )
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 179 (0.76% )
RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 25 (0.11% )
MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 18 (0.08% )
DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 18 (0.08% )
SPOILT VOTES 860 3.64% TOTALS 23,638 100.00%
----------------------------

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO : BUKOBA MJINI

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 117 (0.35%)
KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 15,410 (46.56%)
SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 16,604 (50.16%)
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 449 (1.36%)
RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 14 (0.04%)
MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 14 (0.04%)
DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 9 (0.03%)
SPOILT VOTES 482 1.46%
TOTALS 33,099 100.00%
----------------------------

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO : MTWARA MJINI

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 161 (0.54%)
KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 18,087 (61.04%)
SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 4,415 (14.90%)
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 6,198 (20.92%)
RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 56 (0.19%)
MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 77 (0.26%)
DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 33 (0.11%)
SPOILT VOTES 604 2.04%
TOTALS 29,631 100.00%
----------------------------

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO : TUMBE

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 33 (0.40%)
KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 633 7.64%
SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 59 0.71%
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 7,021 84.71%
RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 127 1.53%
MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 36 0.43%
DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 45 0.54%
SPOILT VOTES 334 4.03%
TOTALS 8,288 100.00%
----------------------------

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO : KOROGWE MJINI

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 110 0.75%
KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 10,761 72.98%
SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 3,135 21.26%
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 394 2.67%
RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 19 0.13%
MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 5 0.03%
DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 6 0.04%
SPOILT VOTES 316 2.14%
TOTALS 14,746 100.00%
----------------------------

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO : KONDE

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 20 0.27%
KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 775 10.58%
SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 45 0.61%
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 6,181 84.35%
RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 66 0.90%
MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 21 0.29%
DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 27 0.37%
SPOILT VOTES 193 2.63%
TOTALS 7,328 100.00%
----------------------------

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO: BABATI MJINI

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 121 (0.58%)
KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 12,699 (60.71%)
SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 7,582 (36.25%)
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 102 (0.49%)
RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 20 (0.10%)
MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 15 (0.07%)
DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 11 (0.05%)
SPOILT VOTES 366 1.75%
TOTALS 20,916 100.00%
----------------------------

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO: MGOGONI

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 22 0.30%
KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 696 9.54%
SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 50 0.69%
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 6,044 82.84%
RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 79 1.08%
MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 23 0.32%
DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 27 0.37%
SPOILT VOTES 355 4.87%
TOTALS 7,296 100.00%
----------------------------

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO: BABATI MJINI

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 121 0.58%
KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 12,699 60.71%
SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 7,582 36.25%
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 102 0.49%
RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 20 0.10%
MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 15 0.07%
DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 11 0.05%
SPOILT VOTES 366 1.75%
TOTALS 20,916 100.00%
----------------------------

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO : NJOMBE KUSINI

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 250 0.83%
KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 22,337 74.43%
SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 6,848 22.82%
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 80 0.27%
RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 32 0.11%
MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 12 0.04%
DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 36 0.12%
SPOILT VOTES 416 1.39%
TOTALS 30,011 100.00%
----------------------------

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO JIMBO: SINGIDA MJINI

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 93 0.36%
KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 19,246 73.64%
SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 5,266 20.15%
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 922 3.53%
RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 21 0.08%
MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 24 0.09%
DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 22 0.08%
SPOILT VOTES 542 2.07%
TOTALS 26,136 100.00%
----------------------------

 
 
MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO JIMBO: MICHEWENI

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 34 0.41%
KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 1,561 18.67%
SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 115 1.38%
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 5,674 67.85%
RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 198 2.37%
MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 64 0.77%
DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 98 1.17%
SPOILT VOTES 618 7.39%
TOTALS 8,362 100.00%



Maswa ni ya Chadema

Wagombea wa Ubunge kupitia chama cha Chadema katika majimbo ya Maswa magharibi na mashariki wameshinda ubunge

Maswa mashariki mgombea alikuwa . Mh. John Magale Shibuda
Maswa mashariki mgombea alikuwa   Mh.Silvester Kasurumbai

Monica Mbega Chali-Iringa Mjini

Mgombea wa Ubunge kwa Tiket ya Chama cha Chadema Mchungaji Peter Msigwa ameibuka mshindi katika jimbo la Iringa Mjini na kumbwaga mpinzani wake kwa tiketi ya chama cha CCM , mama Monica Mbega

ZANZIBAR NI CUF AU CCM ?

Kuna unshindani mkubwa kati ya Cuf na Ccm kwa upande wa zanzibar
JIMBO LA KOROGWE MJINI


JK – 10,761 (72%)


SLAA – 3135 (21.26%)


LIPUMBA - 394 (2.67%)





JIMBO LA NJOMBE KUSINI


JK – 22, 337(74.43%)


SLAA – 6, 848 (22.82%)


LIPUMBA - 80 (0.27%)




JIMBO LA KOROGWE MJINI


JK – (72%)


SLAA –(21.26%)


LIPUMBA - (2.67%)




JIMBO LA TUNGE (ZNZ)


JK – 933 (7.94%)


SLAA –59 (0.71%)


LIPUMBA – 7,021 (84.71%)






JIMBO LA BABATI MJINI


JK – 12, 696 (60.71%)


SLAA – 7,582 (36.52%)


LIPUMBA - 102 (0.49%)





JIMBO LA MTWARA MJINI


JK – 18,087 (61.04%)


SLAA –4,415 (14.6%)


LIPUMBA – 6, 198 ( 20. %)




Jimbo micheweni zanzibar

Kiwete – 18%

Slaa – 1%

Lipumba – 67%


KONDE ZANZIBAR

JK – 10%

SLAA – 0.61%

LIPUMBA – 84.35%


SINGIDA MJINI

JK – 73%

SLAA – 20.5%

LIPUMBA - 3%


MGOGONI ZANZIBAR

JK – 696 (9.54%)

SLAA – 50 (0.96.26%)

LIPUMBA – 6,044 (82.84%)



JIMBO LA BUKOBA MJINI

JK – 15, 410 (46.56%)

SLAA – 16, 604 (50.61%)

LIPUMBA -449 (1.36%)

Chadema na CCM, kazi ipo Arusha !!!

MATOKEO ya awali ya uchaguzi mkuu katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Zanzibar yanaonesha CCM na Chadema kuchuana katika urais, udiwani na ubunge Bara huku CCM na CUF wakichuana Visiwani.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Rajab Kiravu, amesema matokeo rasmi ya urais yanatarajiwa kutolewa keshokutwa.

Katika Jimbo la Kawe mkoani Dar es Salaam katika kata ya Msasani vituo vitano vya Tirdo, Jakaya Kikwete wa CCM anaongoza kwa kupata kura 392, Dk. Willibrod Slaa (Chadema) 237, Hashim Rungwe (NCCR- Mageuzi (1 ) na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF (90).

Katika ubunge, mgombea wa CCM, Angela Kizigha (343), Halima Mdee wa Chadema (228), Mathayo Shaban wa CUF (103), James Mbatia wa NCCR-Mageuzi (36) na Nathaniel Mlaki wa APPT-Maendeleo kura mbili.

Katika kituo cha Tirdo C3, katika urais CCM ilipata kura 75, CUF 25, Chadema 40, APPT moja na vyama vingine sifuri.

Kutoka kata ya Sinza kituo cha Nice, urais CCM (373), Chadema (537) na katika ubunge, Mgombea wa CCM, Hawa Ng’humbi kura 275, mgombea wa Chadema John Mnyika (607).

Katika kituo cha Zahanati Ubungo, katika urais, CCM (203), Chadema (21). Katika ubunge, Ng’humbi wa CCM (111), Mnyika wa Chadema 237 na Julius Mtatiro wa CUF kura 47.

Katika kata ya Jangwani, katika urais, CCM (462), Chadema (110) na CUF (115). Katika ubunge, Mussa Zungu wa CCM (419), Naomi Kaihula wa Chadema (111). Kata ya Segerea, urais CCM (846), Chadema (482) na CUF (717).

Kutoka Arusha, kata ya Kaloleni kituo cha A1, urais CCM (59), Chadema (112), CUF (4) na wengine hawakupata kitu. Katika Ubunge, Dk. Batilda Buriani wa CCM (54), Godbless Lema wa Chadema (113), Balawi Balawi wa CUF (4), Maximilian Lyimo wa TLP (1).

Kituo cha A2 urais CCM (76), Chadema (119), CUF (2) na vyama vingine havikupata kitu. Katika ubunge CCM (71), Chadema (120), CUF (2) na TLP (4).

Katika kituo cha A3 urais CCM (67), Chadema (104), CUF (1) na katika ubunge CCM (62), Chadema (109) na TLP (2).

Kituo A4 urais CCM (65), Chadema (109), wengine hawakupata kitu. Katika ubunge, CCM (63), Chadema (111) na CUF (7).

Katika kituo cha B1, urais CCM (67), Chadema (118), CUF (5) na kwenye ubunge CCM (61), Chadema (121), CUF (3) na TLP (4).

Kutoka Zanzibar vyama vya CCM na CUF vimeonekana kutambiana katika maeneo tofauti na ambayo ni ngome za vyama hivyo.

Katika kituo cha Tumekuja watu 1,201 walipiga kura na matokeo; CUF (897), CCM (302), NCCR-Mageuzi (1) na Jahazi (1).

Kituo cha Haile Selassie watu 809 walipiga kura na CUF kupata 675, CCM 332 na AFP kura mbili. Katika kituo cha Vikokotoni, waliopiga kura ni 1,288 huku tatu zikiharibika.

CUF ilipata kura 906, CCM kura 379, Jahazi mbili na AFP kura mbili. Katika kituo cha Malindi watu 1,025 walipiga, ambapo 13 ziliharibika, CUF (837), CCM (174) na NRA (1).

Jimbo la Kikwajuni, CCM ilifanya vizuri katika vituo vingi lakini matokeo yaliyopatikana mara moja ni katika kituo cha Ben Bella ambako jumla ya watu 1,228 walipiga CCM ikapata 910, CUF 317 na NRA moja.

Jimbo la Kiembe Samaki, CCM ilionekana kufanya vizuri ikilinganishwa na mpinzani wake, katika baadhi ya vituo. Katika kituo cha shule ya msingi ya Kiembe Samaki CCM (1,355) na CUF (493).

Jimbo la Mpendae, kituo cha Jang’ombe matokeo ya awali katika vituo kadhaa yalionesha kuwa vyama hivyo vilikabana huku CCM ikiongoza kwa kura kidogo katika vituo vinne ambavyo matokeo yake yalikuwa yanaendelea kutoka.

VICENT NYERERE KIDEDEA

Mgombea Ubunge kupitia chama cha Chadema  katika Jimbo la  Musoma Mjini ,Ndg: Vicent Nyerere ameibuka mshindi katika jimbo kwa kupata kura 21,335 (59.71%),Akifuatiwa na mgombea wa chama cha CCM ,Ndg: Vedasto Mathayo aliyepata kura 14,723 (39.38%).

Mikoa mengine Bado zoezi la kuisabu kura  linaendelea......

MGOMBEA WA URAIS WA ZANZIBAR ANAONGOZA KATIKA MAJIMBO 12 YA MJINI MAGHARIBI


 
                                                         Dr. Ali Mohammed Shein

 TUME ya uchaguzi Zanzibar imetangaza matokeo ya awali ya  nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa  majimbo 15 ya Unguja na mgombea Urais wa Zanzibar kupitia chama cha mapinduzi CCM DK ALI MOHAMED SHEIN ameonekana kung,aa zaidi kwa ushindi wa majimbo mengi kisiwani Humo.
Akisoma matokeo hayo mbele ya waandishi wa habari,waalikwa,waangalizi wa uchaguzi na wananchi katika ukumbi wa matangazo ya matokeo huko katika hoteli ya Bwawani mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar – ZEC – KHATIB  MWINYICHANDE amesema
                                 
  FUONI
Waliojiandikisha 10884
Waliopiga kura 8768 %90.7
Kura halali 8635 %98.5
Zilizoharibika  133 %1.5
DK SHEIN CCM 3746 %43.4
Maalim Seif  CUF 4852 %56.2

                                 DOLE

Waliojiandikisha 8017
Waliopiga kura 4912
Kura halali  6834 %98.4
Zilizoharibika 108% 1.6
DK SHEIN CCM 4777 %69.9
Maalim Seif  CUF 2007 %6.4
Kasim Bakar wa jahazi asilia 16 % 0.1
                         DIMANI            
Waliojiandikisha 12813
Waliopiga kura 11383 %88.8
Kura halali 11298 %68.5
Zilizoharibika  175 % 1.5
dk SHEIN 6225 % 55.5
Maalim Seif  CUF 4898
Tadea na Jahazi asilia wamefuata kw akufungana kwa kura 23

                KIEMBE SAMAKI
Waliojiandikisha  4998
Waliopiga kura 3856 %35.4
Kura halali 3806
Zilizoharibika  50 % 1.3
DK SHEIN CCM 4338
Maalim Seif  CUF 2812
NCCR mageuzi 10
                                      MWANAKWEREKWE 
Waliojiandikisha  8062
Waliopiga kura 7253 %90.3
Kura halali 7178 % 98.4
Zilizoharibika  115 % 1.6
DK SHEIN CCM 4338 % 60.4 2812 % 39 .2 NRA 10 %0.1
Maalim Seif  CUF
                            BUBUBU
Waliojiandikisha  9809
Waliopiga kura 8827
Kura halali 8606
Zilizoharibika  121
DK SHEIN CCM 4458 %51.8
Maalim Seif  CUF 4119 % 47.9
Nra 12 % 0.1
                        MFENESINI
Waliojiandikisha                    7242
Waliopiga kura                             6203% 85.7
Kura halali                                       6038
Zilizoharibika                                             165
DK SHEIN CCM                                3755 %62.2
Maalim Seif  CUF                                 2246%37.2
AFP 11 %0.2
                                  AMANI
Waliojiandikisha  7641                
Waliopiga kura     6857%                      
Kura halali                6725                     
Zilizoharibika         112 %1.6                                 
DK SHEIN CCM    4567 % 64.9                         
Maalim Seif  CUF  2312 %34.4                             
                                Raha leo
Waliojiandikisha     7229             
Waliopiga kura  6399 %88.5                         
Kura halali        6300 %88.5                             
Zilizoharibika   99 %1.5                                        
DK SHEIN CCM  4043 %64.2            
           
Maalim Seif  CUF     2216 %35.2                           
                                    KIKWAJUNI
Waliojiandikisha     7910            
Waliopiga kura            6513   %82.3                      
Kura halali        6431%98.7
Zilizoharibika  82 % 1.3
DK SHEIN CCM           4534 %70.5
Maalim Seif  CUF   1860 % 28.9
                                      KWAHANI

Waliojiandikisha     7497            
Waliopiga kura     6459%86.2                      
Kura halali        6398 %99.1
Zilizoharibika   61 %0.9
DK SHEIN CCM  4994%78.1
Maalim Seif  CUF     1349 %21.1

                                 MJI MKONGWE

Waliojiandikisha     7495            
Waliopiga kura          6414 %85.6                 
Kura halali        6334 %98.8
Zilizoharibika   80 %1.2
DK SHEIN CCM  1589 %25.1
Maalim Seif  CUF     4717 %74.5
                                      
                          MAGOGONI
Waliojiandikisha 10101                 
Waliopiga kura                           
Kura halali      
Zilizoharibika 
DK SHEIN CCM  3867 %44.1
Maalim Seif  CUF  4867 %55.4 
                       
             
MPENDAE
Waliojiandikisha      9459           
Waliopiga kura   8596 %90.9                         
Kura halali        8476
Zilizoharibika   120
DK SHEIN CCM  4870 %57.5
Maalim Seif  CUF     3546 %41.8
 
                 CHWAKA
CCM    7365      81%
CUF    1610     17.7%
 
                MUYUNI
CCM       6052   81%
CUF    1316     17.7 %
                                      
                 KOANI
CCM       7247    69.3%
CUF   3099     29.7%
 
                   MAKUNDUCHI   
CCM     6544    83%
CUF      1256   15.9 %
DONGE
AFP KURA 9, CCM-6320=88.4, CUF 773=10.8, JAHAZI ASILIA 28=0.1, NCCR-MAGEUZI 5=01%, NRA 5=0.1%, TADEA 11=0.2%

                                       UZINI
AFP 14=0.2%, CCM 7158=89.9%, CUF 731, JAHAZI 29=0.3%, NCCR-MAGEUZI 7=0.1, NRA 8=0.1%, TADEA 12=0.2
 

Sunday, October 31, 2010

JK na Mama Salma wakipiga kura leo



JK akipiga kura yake katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Msoga, kata ya Msoga,Chalinze leo asubuhi.
JK akionyesha wino uliopo katika kidole chake ikiwa ni ishara ya kuonyesha kuwa keshapiga kura leo.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga kura katika kituo cha shule ya msingi Msoga iliopo Chalinze leo asubuhi.
 




Dr. Shein akipiga kura leo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein akipiga kura kwenye kituo cha Uchaguzi Shule ya Msingi Oyesterbay jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein akisalimiana na mmoja wa Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Visiwa vya Ushelisheli walipokutana kwenye Kituo cha Uchaguzi Shule ya Msingi Oyesterbay wakati Makamu wa Rais alipokuja kupiga kura. wa tatu kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ndg. Jordan Rugimbana akisikiliza mazungumzo hayo jijini Dar es Salaam.

  Mh. warioba akipiga kura leo
 
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Joseph Sinde Warioba akipiga kura kwenye kituo cha uchaguzi Shule ya Msingi Oyesterbay jijini Dar es Salaam leo.

Dr Salim katika zoezi la kupiga kura mjini dar leo




Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr. Salim Ahmed Salim, akipiga kura leo jijini Dar es salaam ya kumchagua Rais , Mbunge na Diwani. Dkt Salim aliwasili katika Eneo la Soko la Samaki Msasani saa 12.50 Asubuhi na kufanikiwa kupiga kura katika Kituo B 3 cha Soko la Samaki Msasani saa 1.30 Asubuhi.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr. Salim Ahmed Salim akisubiri Kitambulisho chake kutoka kwa Karani wakati Karani huyo akiendelea na uhakiki ili kudhibitisha kama kweli jina lake limo katika daftari la wapiga kura ili aweze kwenda kupata katarasi za majina ya wagombea ili kushiriki zoezi la upigaji kura za kumchagua Rais, Mbunge na Diwani.

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Salim Ahmed Salim, (wa pili kutoka mwisho) akiwa katika mstari unaolekea katika Chumba cha upigaji kura leo jijini Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki zoezi la kumchagua Rais, Mbunge na Diwani.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO.
 

DENT WA CHUO AKWAMA KUPIGA KURA

Mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu jijini Dar es salaam, ambaye jina lake halikuweza kunaswa mara moja (kushoto) amekwama kupiga kura katika kituo cha Gongolamboto Mwisho baada ya jina lake kutoonekana kwenye orodha ya wasimamizi. Pichani anaonekana akitoa malalamiko yake kwa mwanahabari kutoka kituo cha televisheni kimoja cha jijini Dar.


Msimamizi msaidizi wa kituo cha Gongolamboto Mwisho akitoa maelezo kwa wanahabari kuhusu baadhi ya wapiga kura kutoona majina yao kituoni kwake.


upigaji kura umeanza

Upigaji kura umeanza leo katika maeneo mbalimbali, Usalama na utulivu ktk vituo vingi ni mzuri japo matatizo yaliyoonekana katika sehem mbalimabali ni kwa wapiga kura kutoona majina yao vituoni hali ambayo inaleta usumbufu mkubwa kwa wananchi.

 Iringa:
 mjini iringa hali sio shwari sana ,kwani mbunge mmoja alikuja na gari lake likiwa na picha za wagombea ,kitondo ambacho kinaashilia ni kupiga kampeni wakati sio wakati wa kampeni ata ivyo polisi walimkamata na baadae kuachiwa baada ya kuondoa izo picha na mabango katika gari yake.

Pia wanachi wengi walipata usumbufu wa kutoona majina yao katika vituo vyao hali ambayo imeleta usumbufu mkubwa kwa kuambiwa wakaangalie vituo vingine.

Mwanza:

Jijini mwanza hali ni shwari, watu wengi wamejitokeza kupiga kura mapema asubuhi. zoezi mpaka sasa linaendelea vizuri.

Karatu:
Mgombea uraisi kwa kupitia chama cha chadema mhe. Dr slaa aliingia na helikopta kupiga kura,lakini hali ilikuwa ni tofauti kidogo kwani hakupokelewa na wananchi wengi kama ilivyokuwa kipindi cha kampeni.
Watu wengi waliona majina yao vituoni, nakuaza kuendelea na upigaji kura kwa amani.

Mtwara:
Jimboni Tandahimba,kuna tukio la katibu wa tawi wa chama kimoja kachomewa moto nyumba yake jana usiku, Pia kuna kundi la watu linaweka magogo njianai ili kuzuia wananchi wasiende kupiga kula, kwa ufupi hali sio shwari sana.

Mtwara mjini: kiongozi wa chama kimoja kafanya hujuma ya fujo kwa mgombe mwenzake,polisi walimkamata na baadae kuachiwa huru kwa dhamana.

Mtu mwengine kakamatwa akitoa rushwa ya kugawa mchele kwa wananchi.

Taarifa zengine tutakuletea kadri tutakapozipata , na kama unataarifa yoyote kuhusu maandeleo ya upigaji kura tutumie kwa email hii : bkipira@gmail.com