Home

HOME I

Sunday, October 31, 2010

JK na Mama Salma wakipiga kura leo



JK akipiga kura yake katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Msoga, kata ya Msoga,Chalinze leo asubuhi.
JK akionyesha wino uliopo katika kidole chake ikiwa ni ishara ya kuonyesha kuwa keshapiga kura leo.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga kura katika kituo cha shule ya msingi Msoga iliopo Chalinze leo asubuhi.
 




Dr. Shein akipiga kura leo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein akipiga kura kwenye kituo cha Uchaguzi Shule ya Msingi Oyesterbay jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein akisalimiana na mmoja wa Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Visiwa vya Ushelisheli walipokutana kwenye Kituo cha Uchaguzi Shule ya Msingi Oyesterbay wakati Makamu wa Rais alipokuja kupiga kura. wa tatu kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ndg. Jordan Rugimbana akisikiliza mazungumzo hayo jijini Dar es Salaam.

  Mh. warioba akipiga kura leo
 
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Joseph Sinde Warioba akipiga kura kwenye kituo cha uchaguzi Shule ya Msingi Oyesterbay jijini Dar es Salaam leo.

Dr Salim katika zoezi la kupiga kura mjini dar leo




Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr. Salim Ahmed Salim, akipiga kura leo jijini Dar es salaam ya kumchagua Rais , Mbunge na Diwani. Dkt Salim aliwasili katika Eneo la Soko la Samaki Msasani saa 12.50 Asubuhi na kufanikiwa kupiga kura katika Kituo B 3 cha Soko la Samaki Msasani saa 1.30 Asubuhi.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr. Salim Ahmed Salim akisubiri Kitambulisho chake kutoka kwa Karani wakati Karani huyo akiendelea na uhakiki ili kudhibitisha kama kweli jina lake limo katika daftari la wapiga kura ili aweze kwenda kupata katarasi za majina ya wagombea ili kushiriki zoezi la upigaji kura za kumchagua Rais, Mbunge na Diwani.

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Salim Ahmed Salim, (wa pili kutoka mwisho) akiwa katika mstari unaolekea katika Chumba cha upigaji kura leo jijini Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki zoezi la kumchagua Rais, Mbunge na Diwani.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO.
 

No comments: