Home

HOME I

Tuesday, November 2, 2010

Rais mpya wa zanzibar ni Dk Ali mohamed shein

Rais Mteule, Dk. Shein kupitia CCM ameshinda kwa jumla ya kura 179, 809 sawa na 50.1% ya kura zote, il hali Maalim Seif kupitia CUF amepata kura 176, 538 sawa na 49.1% na zilizobaki ni za vyama vingine.

Maalimu Seif pia ameipongeza tume ya uchaguzi ya Zanzibar, ZEC, kwa zoezi la uchaguzi, lakini pia ametoa maoni juu ya mapungufu aliyoyaona hasa kuhusu shahada za kupiga kura na matumizi ya mabavu kwa mawakala wa vyama na watu mbalimbali wanapohoji na kutaka taarifa sahihi. Amemsihi Rais Mteule alishughulikie suala hilo. Kabla ya kuhitimisha hotuba yake fupi, Malim Seif alisema kuwa katika matokeo haya, "hakuna mshindi wala mshindwa" kwani washindi ni Wazanzibari na imani yake ni kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa italeta mafanikio nchini humo. Amemsihi Rais Mteule kuwaasa watu kuacha kubezana, kwani kufanya h ivyo kunaweza kusabababisha mtafaruku. Baada ya kuzungumza, Malim Seif alinyanyuka na kumpa mkono wa pongezi Rais Mteule wa Zanzibar, 2010 - 2015, Dk. Ali Mohamed Shein.

Ilipofika zamu ya Rais Mteule kuzungumza, naye alitoa pongezi kwa Maalim Seif na kupongeza zoezi zima la uchaguzi jinsi lilivyoendekea. Pia ametoa ahadi ya kushirikiana na wote katika ujenzi wa Zanzibar mpya kwa mujibu wa maridhiano mapya ya uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar.

No comments: