MATOKEO ya awali ya uchaguzi mkuu katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Zanzibar yanaonesha CCM na Chadema kuchuana katika urais, udiwani na ubunge Bara huku CCM na CUF wakichuana Visiwani.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Rajab Kiravu, amesema matokeo rasmi ya urais yanatarajiwa kutolewa keshokutwa.
Katika Jimbo la Kawe mkoani Dar es Salaam katika kata ya Msasani vituo vitano vya Tirdo, Jakaya Kikwete wa CCM anaongoza kwa kupata kura 392, Dk. Willibrod Slaa (Chadema) 237, Hashim Rungwe (NCCR- Mageuzi (1 ) na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF (90).
Katika ubunge, mgombea wa CCM, Angela Kizigha (343), Halima Mdee wa Chadema (228), Mathayo Shaban wa CUF (103), James Mbatia wa NCCR-Mageuzi (36) na Nathaniel Mlaki wa APPT-Maendeleo kura mbili.
Katika kituo cha Tirdo C3, katika urais CCM ilipata kura 75, CUF 25, Chadema 40, APPT moja na vyama vingine sifuri.
Kutoka kata ya Sinza kituo cha Nice, urais CCM (373), Chadema (537) na katika ubunge, Mgombea wa CCM, Hawa Ng’humbi kura 275, mgombea wa Chadema John Mnyika (607).
Katika kituo cha Zahanati Ubungo, katika urais, CCM (203), Chadema (21). Katika ubunge, Ng’humbi wa CCM (111), Mnyika wa Chadema 237 na Julius Mtatiro wa CUF kura 47.
Katika kata ya Jangwani, katika urais, CCM (462), Chadema (110) na CUF (115). Katika ubunge, Mussa Zungu wa CCM (419), Naomi Kaihula wa Chadema (111). Kata ya Segerea, urais CCM (846), Chadema (482) na CUF (717).
Kutoka Arusha, kata ya Kaloleni kituo cha A1, urais CCM (59), Chadema (112), CUF (4) na wengine hawakupata kitu. Katika Ubunge, Dk. Batilda Buriani wa CCM (54), Godbless Lema wa Chadema (113), Balawi Balawi wa CUF (4), Maximilian Lyimo wa TLP (1).
Kituo cha A2 urais CCM (76), Chadema (119), CUF (2) na vyama vingine havikupata kitu. Katika ubunge CCM (71), Chadema (120), CUF (2) na TLP (4).
Katika kituo cha A3 urais CCM (67), Chadema (104), CUF (1) na katika ubunge CCM (62), Chadema (109) na TLP (2).
Kituo A4 urais CCM (65), Chadema (109), wengine hawakupata kitu. Katika ubunge, CCM (63), Chadema (111) na CUF (7).
Katika kituo cha B1, urais CCM (67), Chadema (118), CUF (5) na kwenye ubunge CCM (61), Chadema (121), CUF (3) na TLP (4).
Kutoka Zanzibar vyama vya CCM na CUF vimeonekana kutambiana katika maeneo tofauti na ambayo ni ngome za vyama hivyo.
Katika kituo cha Tumekuja watu 1,201 walipiga kura na matokeo; CUF (897), CCM (302), NCCR-Mageuzi (1) na Jahazi (1).
Kituo cha Haile Selassie watu 809 walipiga kura na CUF kupata 675, CCM 332 na AFP kura mbili. Katika kituo cha Vikokotoni, waliopiga kura ni 1,288 huku tatu zikiharibika.
CUF ilipata kura 906, CCM kura 379, Jahazi mbili na AFP kura mbili. Katika kituo cha Malindi watu 1,025 walipiga, ambapo 13 ziliharibika, CUF (837), CCM (174) na NRA (1).
Jimbo la Kikwajuni, CCM ilifanya vizuri katika vituo vingi lakini matokeo yaliyopatikana mara moja ni katika kituo cha Ben Bella ambako jumla ya watu 1,228 walipiga CCM ikapata 910, CUF 317 na NRA moja.
Jimbo la Kiembe Samaki, CCM ilionekana kufanya vizuri ikilinganishwa na mpinzani wake, katika baadhi ya vituo. Katika kituo cha shule ya msingi ya Kiembe Samaki CCM (1,355) na CUF (493).
Jimbo la Mpendae, kituo cha Jang’ombe matokeo ya awali katika vituo kadhaa yalionesha kuwa vyama hivyo vilikabana huku CCM ikiongoza kwa kura kidogo katika vituo vinne ambavyo matokeo yake yalikuwa yanaendelea kutoka.
No comments:
Post a Comment