Home

HOME I

Wednesday, June 8, 2011

TCAA sasa kuboresha maslahi ya wafanyakazi.




MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), inakusudia kuboresha maslahi ya wafanyakazi kutokana na mamlaka hiyo kufanya vizuri kwa miaka miwili mfululizo. Akizungumza kwenye hafla ya kupongeza wafanyakazi bora wa mamlaka hiyo juzi, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Fadhil Manongi, alisema kwa miaka miwili mfululizo wamefanya vizuri na kuna maendeleo ya utendaji, hivyo siyo busara maslahi ya wafanyakazi kuendelea kuwa duni.

“Mara kwa mara tumekuwa tukizungumzia kuboresha maslahi yenu na kwa miaka miwili mfululizo tumeonekana tuna maendeleo, hivyo tutaboresha maslahi,” alisema Manongi.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (Tughe) tawi la TCAA, Eugene Lwalwa, alisema kwa miaka saba mfululizo mamlaka hiyo imeongoza kwa kutoa wafanyakazi bora kitaifa. Lwalwa aliwataka waajiri nchini kuboresha maslahi ya wafanyakazi wao hasa pale wanapotoa huduma bora zaidi.

 Katika sherehe hizo wafanyakazi 23 walitunukiwa vyeti na Sh400,000 kila mmoja,  kati yao 11 wanatoka Dar es Salaam na wengine mikoani.

1 comment:

kipira said...

usiseme vitu ambavyo havijafanyiwa utafiti usije ukawa kama wabunge wa chama tawala, kuboreshwa kwa maslai ni pamoja na kurekebisha scheme mbovu za TCAA nani anaweza kusimama kifua mbele na aseme kweli scheme of service zimeboreeshwa utasemaje mazingira mazuri kama kada zingine mtu anatumika miaka ishirini bila mafanikio au hivyo ndo mnapenda? Haina shida nyie watu wa operation endeleeni kututengenezea ulaji sisi tutatumia pesa mnayoizalisha na nyie tutawapa ufanyakazi bora wakati sisi tunachukua posho nzuri kwenye vikao na mishahari mizuri pia tutapitisha mapendekezo yale ambayo yanatuzingatia sisi zaidi mfano hali bora, umeona tunazungumza habari za stesheni allowance? Tuwape ili safari zetu zife? kaeni huko hata training tutawapeleka CATC