Home

HOME I

Sunday, November 7, 2010

KIKWETE ASHINDA URAISI KWA 61.7%



                                                                      
                                   
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)  ilimtangaza Kikwete aliyekuwa akigombea nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM, kuwa mshindi baada ya kupata kura 5,276,827 (sawa na  61.17%) ya kura zote halali zilizopigwa 8,626,283.

Akitangaza matokeo hayo Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Lewis Makame, alisema Kikwete alipata ushindi huo, miongoni mwa wagombea wa vyama saba vya siasa waliowania.

Aliyekuwa mgombea wa Chadema, Dk Willibrod Slaa hakuhudhuria hafla hiyo kutokana na kile alichodai juzi kuwa hakubaliani na matokeo.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, nafasi ya pili katika kinyang’anyiro hicho ilichukuliwa na Willibrod Slaa wa Chadema ambaye alipata kura 2,271,941 (sawa na 26.34%) ya kura zote halali.

Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 695,667 (sawa na  8.06% ) ya kura zote halali.

Baada ya kutangaza matokeo hayo, Rais Kikwete aliwashukuru wapiga kura, NEC na vyombo vya habari kwa kuwezesha uchaguzi huo kufanyika kwa utulivu na amani.

Alisema, “ushindi niliopata unaonesha imani ya wapiga kura kwangu na ninaahidi nitawatumikia kwa ari mpya zaidi, nguvu mpya zaidi na kasi mpya zaidi.” .

No comments: