Home

HOME I

Thursday, October 21, 2010

isha mashauzi atwangwa Talaka

Lile gogoro la staa wa miondoko ya mwambao anayetumika katika Kundi la Jahazi Modern Taarab, Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’ kupigana na mumewe, limefungua sura mpya baada ya mwanaume huyo, Jumanne Hassan ‘Tevez’ kumtwanga talaka mkewe huyo.

Talaka hiyo ilitolewa Oktoba 18, 2010 nyumbani kwa wanandoa hao, Tandale-Kwatumbo, Dar na kushuhudiwa na wanandugu kadhaa wa pande zote mbili akiwemo mama mzazi wa Isha.


Baada ya kuzinyaka taarifa hizo, Amani lilifika nyumbani kwao na kufanikiwa kumkuta Isha Mashauzi na mama yake mzazi, Rukia Juma wakiwa wamekaa nje kibarazani kwa kile kilichosemekana kwamba, walikuwa wakimsubiri Tevez.

Ilipotimu saa 7:00 mchana, Tevez alitia timu na kuwakuta wakimsubiri kwani ilidaiwa kuwa, baada ya ugomvi wao wiki moja nyuma, Isha hakuwahi kurudi nyumbani kwake.
Huku Amani likishuhudia, kitendo bila kuchelewa, Tevez alikabidhi talaka kwa mkewe Isha huku akimwamuru achukue kila kitu alichokiona ndani ya nyumba hiyo kwa vile kilikuwa ni haki yake, mama mzazi alikuwa akishuhudia kwa mshangao.
Nyota huyo wa Taarab alionekana kushtuka na kushindwa kuamini macho yake, palepale alimwaga chozi lenye ujazo wa kijiko cha chai na kuanza kufanya mpango wa kutafuta lori la kubebea mizigo yake.

Lori aina ya Canter lilifika na kuegesha kinyumenyume jirani na mlango mkubwa, Isha akisaidiwa na baadhi ya nduguze walianza kutoa vinavyowahusu na kuingiza kwenye gari hilo.

Hata hivyo, ili kumfanya akaanze maisha kwa urahisi kidogo, mwanaume huyo alimpa mtalaka wake huyo kiasi cha Dola za Kiamerika 100 (kama Shilingi 130,000 za Bongo) huku akitamka kuwa, Jumamosi au Jumapili ijayo amtafute ili ammalizie deni la mahari iliyobaki wakati wa mchakato wao wa kuoana.

Zoezi hilo lilipokamilika, Amani liliongea na Tevez kwa njia ya simu yake ya kiganjani lengo likiwa kupata uhakika wa kile kilichotokea ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Kusema ukweli ulichokiona au kuambiwa ni kweli, nimeshindwa kuishi na mke asiyejua kuheshimu ndoa yake. Kikubwa kilichoniuma, wakati alipolazwa hospitali kwa kile kipigo nilichompa, simu yake nilikuwa nayo mimi, nilikuta sms (ujumbe mfupi wa maandishi) nyingi za mapenzi.”
Tevez aliendelea kusema kuwa, meseji hizo zilikuwa zikienda kwa wanaume mbalimbali, nyingine alikuwa akiomba msaada wa kupangishiwa chumba, nyingine akiomba fedha.
Amani lilifanikiwa kuziweka kibindoni meseji hizo sanjari na namba za simu zilizotumiwa. Moja jina lake ‘liliseviwa’ Samir.

Meseji nyingine ilionekana kwenda kwenye namba ambayo Amani lilipoifuatilia liligundua mtumiwaji anaishi nchini Ugiriki. Huyu alikuwa akiombwa kiasi cha pesa ya Ulaya (Euro) 50 kwa minajili ya kulipia kodi ya chumba.
Meseji nyingine ilikwenda kwenye namba ambayo tunaisitiri, lakini kwenye simu iliseviwa kwa jina la Mkurugenzi, mawasiliano yao yalikuwa machafu kupita maelezo.
Katika habari hiyo, wawili hao walitwangana kiasi cha kuumizana na kupasuliana vioo vya magari yao, kisa kikiwa mke kuonesha dalili za kutokuwa mwaminifu katika ndoa.

‘Vita’ hiyo ilimfanya Isha kulazwa hospitali ambayo haikujulikana jina mara moja baada ya kuumia vibaya na hali yake kuwa mbaya.

1 comment:

Mponda said...

Nimeupenda huu udaku