Home

HOME I

Sunday, October 31, 2010

upigaji kura umeanza

Upigaji kura umeanza leo katika maeneo mbalimbali, Usalama na utulivu ktk vituo vingi ni mzuri japo matatizo yaliyoonekana katika sehem mbalimabali ni kwa wapiga kura kutoona majina yao vituoni hali ambayo inaleta usumbufu mkubwa kwa wananchi.

 Iringa:
 mjini iringa hali sio shwari sana ,kwani mbunge mmoja alikuja na gari lake likiwa na picha za wagombea ,kitondo ambacho kinaashilia ni kupiga kampeni wakati sio wakati wa kampeni ata ivyo polisi walimkamata na baadae kuachiwa baada ya kuondoa izo picha na mabango katika gari yake.

Pia wanachi wengi walipata usumbufu wa kutoona majina yao katika vituo vyao hali ambayo imeleta usumbufu mkubwa kwa kuambiwa wakaangalie vituo vingine.

Mwanza:

Jijini mwanza hali ni shwari, watu wengi wamejitokeza kupiga kura mapema asubuhi. zoezi mpaka sasa linaendelea vizuri.

Karatu:
Mgombea uraisi kwa kupitia chama cha chadema mhe. Dr slaa aliingia na helikopta kupiga kura,lakini hali ilikuwa ni tofauti kidogo kwani hakupokelewa na wananchi wengi kama ilivyokuwa kipindi cha kampeni.
Watu wengi waliona majina yao vituoni, nakuaza kuendelea na upigaji kura kwa amani.

Mtwara:
Jimboni Tandahimba,kuna tukio la katibu wa tawi wa chama kimoja kachomewa moto nyumba yake jana usiku, Pia kuna kundi la watu linaweka magogo njianai ili kuzuia wananchi wasiende kupiga kula, kwa ufupi hali sio shwari sana.

Mtwara mjini: kiongozi wa chama kimoja kafanya hujuma ya fujo kwa mgombe mwenzake,polisi walimkamata na baadae kuachiwa huru kwa dhamana.

Mtu mwengine kakamatwa akitoa rushwa ya kugawa mchele kwa wananchi.

Taarifa zengine tutakuletea kadri tutakapozipata , na kama unataarifa yoyote kuhusu maandeleo ya upigaji kura tutumie kwa email hii : bkipira@gmail.com

1 comment:

Mponda said...

Hili swala la kupoteza majina wamelifanya kwa makusudi ili kupunguza idadi ya wapiga kura. Jana nilimsikia mkuu wa NEC akisema kuwa mambo yote shwari je hii ndo shwari kweli. Aaache uongo